Noti ya Elfu Kumi Yamtesa Soudy Brown .
Moja ya viongozi wa kituo cha polisi amethibitisha taarifa kuwa msanii Maua Sama pamoja na mtangazaji wa Clouds Media Soudy brown wamekamatwa na polisi siku ya jana wakituhumiwa kwa kosa la kuidharirisha pesa ya serikali.
Mtu wa kwanza kutoa taarifa hiyo alikuwa ni mtayarishaji wa muziki Abbah ambae alisema kuwa Maua Sama pamoja na Soudy brown walikuwa wote ndani lakini baadae yeye alitolewa na kuwaacha wenzake ndani.
Hata hivyo baada ya hapo kiongozi wa kituo cha polisi walichokamatwa wasanii hao alithibitisha swala hilo na kusema kuwa “ni kweli hawa watu tunao na tumewaweka ndani, mwingine jana na mwingine leo lakini kwa sasa tumewashikilia watu hawa na tunatafuta wapelelezi wa kesi hiyo .
Hata hivyo polisi huyo anasema kuwa kosa kubwa walilofanya watu hawa ni kudharirisha pesa ya serikali kutokana na video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha maua sama akiwa anakanyaga pesa ya noti ya shilingi elfu 10.