“Nitafanya Chochote Ilimradi Nikuone Unatabasamu” Jux Amfungukia Vanessa
Penzi la Wanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee na Juma Jux linaonekana kumea na kuchanua kila siku hadi kufikia hatua ya wawili hawa kushindwa kujizuia na hisia zao.
Hakuna safari ya mapenzi iliyonyooka lazima kunakuwa na milima na mabonde mtakayo kutana nayo lakini mkiyavuka salama mwisho wa siku mtamaliza safari yenu, hili limethibitishwa na moja was kati ya couple kali bongo inayoundwa na mastaa wote.
Jux na Vanessa walianza mahusiano yao miaka michache iliyopita lakini baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miaka minne mwaka jana walitangaza kuwa wameachana ingawa hawakuweka wazi sababu kamili iliyopelekea kutengana kwao tetesi nyingi zilikuwa michepuko.
Kwenye mahojiano mbali mbali ambayo Vanessa alifanya alisisitiza kuwa kamwe hawezi kirudiana na mtu ambaye ameachana naye lakini tetesi za kurudiana zilianza kutawala mitandao ya kijamii walipoanza kufanya ziara ya tamasha la Fiesta ingawa walikataa siku za mwanzoni lakini mwishoni walikubali.
Tangu wapendanao hawa wamerudiana kwa mara nyingine wamekuwa na ukaribu wa ajabu kwani kila sehemu wako wote na kila mmoja amekuwa akifunguka mahaba aliyonayo kwa mwenzake kupitia mitandao ya kijamii.
Weekend iliyopita Vanessa na Jux walisafiri na kuenda visiwani Zanzibar kula bata na hawakusita kuwaonyesha mashabiki zao jinsi wanavyokula raha na mahaba mazito, ambapo maneno kama nakupenda yakiwa yametawala na kadhalika.
Jux aliweka picha ya Vanessa kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuisindikiza kwa maneno haya. “I will do anything to make you smile #prevalentines” na Vanessa alimjibu kwa kumwekea mabusu kibao. Kuna habari zimekuwa zikidai kuwa Vanessa ni mjamzito na wawili hao wanategemea kupata mtoto lakini hakuna aliyethobitisha habari hizo.