Nisha Hataki Tena Wanaume wa Bongo
Msanii wa maigizo na vichekesho Salma Jabu maarufu kaa nisha amesema kuwa kwa sasa hataki tena kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume wa kibongo kwa sababu wana mapenzi ya kuigiza ambayo kwake anaona yanampotezea muda na kumuumiza.
Nisha anakiri kuwa kwa muda mrefu sasa amekuwa katika mapenzi na wanaume wa kibongo tofauti tofauti na amekuwa akiumizwa kila kukicha hivyo amechoka kuumizwa kama anataka kuingia katika mapenzi sasa hivi atataufua mwanamue wa nje ya nchi na sio mbongo tena.
hivi sasa naanzaje kutoka kimapenzi na mwanaume wa kibongo, walivyowaongo na walaghai hivyo.nimepoteza muda mwingi sana katika kuwapenda wanaume wa kibongo na kuwathamini lakini ninachoambulia kwao ni maumivu na fedhea.
Nisha amekuwa ni moja ya wasanii wa kike wanaoandikwa sana katika vyombo vya habari kwa maneno ya kuachwa na kuumizwa sana na mapenzi, wanaume wengi anaokuwa nao wanaibiwa na wanawake wenzake na kubaki mpweke,hivyo nisha ameamua kuachana na mapenzi ya mawazo na stress hivyo ameona ni bora kuachana na wabongo kabisa.