“Nipo Tayari Kuzaa na Mtoto Mwingine”-Aunty Ezekiel
Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel ameibuka na kuweka wazi mipango yake kuzaa Mtoto mwingine baada ya binti yake ambaye Hivi sasa ana umri wa miaka minne.
Aunty Ezekiel na Mpenzi wake ambaye ni mnenguaji kutoka label ya WCB, Mose Iyobo, amesema sasa ni wakati wake wa kuongeza mtoto mwingine endapo mipango ya Mungu itatimia.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Aunty Ezekiel amesema kuwa anaona wakati umefika wa kuongeza mtoto wake wa pili:
Nadhani sasa ni wakati sahihi wa kupata mdogo wake Cookie, najua kila kitu ni mipango ya Mungu na hata hili litatimia kwa uwezo wake, nilipanga kuwa na watoto zaidi ya wawili na naamini inawezekana, kama mambo yatakwenda vizuri wakati wowote nitakuwa tayari kwa hilo“.