Nipo Tayari Kufunga Ndoa na Diamond- Lynn
Video vixen maarufu kweNey muziki wa Bongo fleva aliyejizolea umaarufu Kupitia video ya Rayvanny, Irene Godfrey maarufu kama Lynn amesema kuwa yupo tayari kuolewa na Diamond Platnumz na hata mpenzi wake anajua hilo.
Lynn ambaye katika wiki chache Hizi amekamata sana headlines kutokana na tetesi za kuwa Kwenye Mahusiano na Diamond ameibuka na kudai Yupo Tayari kwa ndoa na Bongo Star huyo.
Kwenye mahojiano na Waandishi kwenye red carpet ya Biko Jibebe Challenge, Lynn amesema kama ikitokea nafasi hiyo atakuwa tayari.
Yeah! kwa sababu ni mwanaume, siwezi kusema hapana”.
Lakini pia Lynn alionekana kujikanyaga pale alipobanwa sana na maswali ya Mahusiano na Diamond ikiwemo gari ambalo alilopewa kama zawadi siku ya birthday yake ambalo lilisemekana limetoka kwa Diamond.