Nimepata Somo Kubwa Sana Kutoka Kwa Wanaigeria- Rammy Galis
Msanii wa Bongo movie Rammy Galis amefunguka na kuweka wazi kuwa amejifunza somo kubwa kutoka kwa wasanii wa Nigeria kutokana na tu kufanya nao kazi.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Mwananchi, Rammy Galis amesema kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya wasanii wa Nigeria na Tanzania katika kufanya kazi kwani Wanaigeria ni watu wa kujali muda zaidi na kutbamini kazi bila kujali Mali wanazomiliki.
Wenzetu hawa bila kujali ana jina kubwa kiasi gani kwenye sanaa au anaendesha gari la thamani gani, unapofika muda wa kazi wao wanajali sana wanachokifanya tofauti na wa hapa nyumbani”.
Wanaigeria walimipa somo kubwa sana kwamba kazi inayokupa ugali wa kila siku lazima uiheshimu tofauti na hapa Bongo kisa mtu anaendesha gari zuri na msanii basi atataka umnyenyekee na kufika location wa mwisho ili kila mmoja amtazame anavyofika, tubadilike”.
Rammy Galis anafanya vizuri na filamu yake ya Red Flag aliyoigiza na wasanii wengi wa nchini Nigeria.