Nilikuwa na Ndoto Ya Kuwa Mwanasheria- Gigy Money
Video vixen na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu Kama Gigy Money ameibuka na kudai mbali ya kufanya muziki Lakini Ndoto Yake kubwa ilikuwa kuwa mwanasheria.
Gigy Money ameibuka na kudai kuwa alipokuwa mdogo alikuwa ana Ndoto kila siku za kuja kuwa mwanasheria na sio mwanamuziki kama alivyo Hivi sasa.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Gigy Money amesema kuwa alikua akipenda fani hiyo tangu akiwa mdogo kutokana na kuwa na uwezo wa kumsimamia mtu katika ukweli bila kuyumbishwa.
Nilikua napenda sana sheria, sema sikusoma sana na niliishia kidato cha pili lakini ndoto yangu kubwa ilikua kuja kuwasimamia watu kupata haki zao, mambo ya muziki nimeyavamia tu“.