“Nilijua Hamisa Atakuwa Staa Tangu Zamani”-Mama Mobetto
Mama mzazi wa mwanamitindo na msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto, Shufaa Rutiginga maarufu kama Mama Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa alijua mwanaye atakuwa maarufu tangu akiwa mdogo.
Kwenye mahojiano aliyofanya Global Publishers, Mama Mobetto amesema kuwa mwanaye alionesha mapema atakuwa mtu fulani kutokana na jinsi alivyokuwa akijiweka na watu wengi walimwambia kuwa atakuwa mlimbwende.
Unajua Mobeto alikuwa akijipenda tangu mdogo na alikuwa na mambo f’lani ambayo niliamini akikua atakuwa mtu f’lani mwenye jina mjini”.
Lakini pia Mama huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kuona umaarufu wa mwanaye alijitahidi kumpa malezi mazuri na makini kwani alimlea peke yake bila kuwa na baba.
Mama huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kuona umaarufu wa mwanaye alijitahidi kumpa malezi mazuri na makini kwani alimlea peke yake bila kuwa na baba”.
Mobetto anaendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki kwani wimbo wake wa ‘Tunaendana umeendelea kukamata chati.