Nikki Wa Pili: Ipo siku nataka kugombea uraisi
Mwanamuziki na Rapa maarufu Tanzania kutoka kundi la Weusi anayejulikana kama Nikki wa pili amekiri kuwa moja kati ya ndoto yake kubwa maishani ni kuja kugombea uraisi ili kusaidia nchi yake ya Tanzania kutokana na matatizo ambayo wananchi wanayo na wimbi kubwa la umaskini unaolikabili taifa hili.
Kukiwa na wimbi kubwa la wasanii wa muziki wa Bongo fleva kujiingiza katika fani ya siasa ambayo hayo yameonekana kwa wasanii wakubwa kwenye tasnia hii ikiwemo Mheshimiwa Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya mjini ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo maarufu kwa jina la sanaa kama “Sugu” ambaye aliachana na muziki na kuamua kuingia kwenye siasa. Pia mfano mwingine ni Proffesor Jay ambaye alikuwa ni rapa maarufu sana kwa nyimbo zake naye pia aliamua kuukacha muziki na kuamua kuingia katika siasa ambaye sasa ni Mbunge wa Mikumi lakini pia wasanii wengi wamejaribu kuingia katika siasa kama Wema Sepetu lakini hawakufanikiwa.
Katika mahojiano aliyoyafanya Nikki wa pili hivi karibuni alisema kuwa ni vizuri kwa wasaanii hawa kuingia katika siasa kama wabunge ili kusaidia jamii zao na Watanzania kwa ujumla lakini yeye kwa ubinafsi wake ameona kuwa hatogombania ubunge bali anataka moja kwa moja anataka akagombanie uraisi wa nchi ili apate nafasi kubwa zaidi kutatua matatizo ya wananchi. Mwanamuziki huyo alisisitiza:
“Ipo siku nataka nataka kugombea uraisi kwasababu nitakuwa na nafasi kubwa ya kutatua matatizo ya Watanzania kuliko kuwa mbunge”.