Nikki Wa Pili Azungumzia Bifu La Dogo Janja Na Young Dee
Wakiwa bado wanavuma sana katika vichwa vya habari sehemu mbalimbali wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) msanii Dogo Janja kutoka Arusha na Young Dee kutoka wa Dar Es Salaam kutokana na bifu linaloendelea kati yao katika mitandao na vyombo vya habari , msanii mkongwe na mwenye mafanikio kutoka kundi la Weusi ameamua kulizungumzia bifu ilo ambalo linaonekana ni tatizo .
Nikki amekuwa ni mmoja wa wasanii ambao amekuwa akishauri na kusaidia watu wengi katika tasnia ya muziki na nje ya muziki pia, ukiachana na kipaji cha muziki alichonacho Nikki akiaminika sana katika jamii kutokana na ushawishii wake mkubwa kwa vijana wenzake katika swala zima la maendeleo
Akiongean na eNews ya EATV, Nikki wa Pili anaona kuwa bifu ilo linaendelea na linaweza kufika pabaya ilhali wasanii hao wameanza kuingia katika maisha yao binafsi badala ya kuwa na ushindani wa kikazi “mimi naona kama kuna tatizo hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi,kwaiyo ningefurahi kuona wanashindana kumuziki zaidi.” alisema Nikki wa Pili
Kwa kuongezea pia Nikki aliwashauri kuwa wao kama wasanii maneno mengi wanayoyasema huwa yanabaki kuishi katika jamii na ni vigumu kuyapoteza kwa mara moja hivyo kwa kila jambo wanalofanya au kuongea ni lazima wachagulie lile lililo sahihi ” maana unapokuwa maarufu ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika kirahisi kwa hiyo ni vizuri zaidi kama watachagua maneno ya kutumia kila mara” aliongezea Nikki wa Pili
Dogo Janja na Young Dee waliingia katika bifu zito baada ya Young Dee kukataa kufananishwa na msanii mwenzie Dogo Janja, huku akitoa sababu kuwa yeye ni mkubwa kimuziki kuliko msanii mwenzie huyo, lakini haikuwa rahisi kwa Dogo Janja kukubaliana na kauli ya mwenzie hivyo aliamua kumjibu, katika majibu yake Dogo Janja alimwita Young Dee ‘mteja’ na kwamba hata yeye hawezi kulinganishwa kimuziki na mtu anaekula unga, kitu kilichofanya wawili hao kundelea kuzozana.