Nikki wa pili Awaingiza Wasanii Wenzake Darasani
Msanii Nikki wa pili amefunguka na kuongelea swala la wasanii wengi kuongezeka nchini huku wakiwa na majina makubwa na umaarufu kuliko hata kipato wanachoingiza kutokana na majina yao na uatajiri wao haulingani na vile wanavyoongelewa.
Nikki anasema kuwa wasanii wengi wanahitaji elimu ya masoko ili kuongeza wasanii wenye majina na vipato pia kwa sababu wasanii wengi wamekuwa wakifurahia kupata majina na kusahau kuwa majina hayo yanahitaji nkuendana na utajiri wao.
Nikki wa pli anasema “Kuibali sanaa kuwa kipato ni hata ngumu sana, iwe uchoraji au uchongaji au kitu chochote, wasanii wengi wanabaki na snaa zao kama hobi tu na sio kitu cha kupatia kipato.somo la marketing pia linahitajika sana kwa wasanii branding na huduma kwa wateja pia kwa wasanii ni muhimu pia.
Maneno ya Nikki yanakuja kutokana na ukweli kuwa wasanii wamekuwa wengi na wnegi wamekuwa na majina lakini pesa wanayipata kutokana na sanaa hiyo haiendani na majina yao na hii uthihirika zaidi pale ambapo wasanii wanapopata matatizo kama magonjwa na kujikuta wakiomba misaada sana.