Nikki Wa Pili Amwaga Povu Zito Kwa Wasanii Wakaa Uchi
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Nikki Wa Pili amewaji juu na kuwatolea povu zito mastaa ambao wameandamwa na skendo ya kuweka picha na video chafu zenye maudhui yasiyo ya kimaadili kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nikki wa Pili amewachana watu hasa wasanii wanaotafuta kiki kupitia vitu visivyo na maana.
https://www.instagram.com/p/BpYt1DMjQna/?utm_source=ig_web_copy_link
Amber Rutty, Wema Sepetu na Gigy Money ni baadhi tu ya mastaa ambao hivi sasa wanatengeneza headlines kwa vitendo vyao vya kuachia picha chafu kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi yao wameshachukuliwa hatua za kisheria.