Nikki Mbishi na Moni Centrozone Ndani ya Bifu Zito.
Wasanii wa muziki wa kufoka foka Moni pamoja na Nikki wa Mbishi wameendelea kutupiana maneno katika mtandao ya kijamii baada ya nikki mbishi kusema siku chache zilizopita kuwa kundi jipya la Moni pamoja na Country Boy litakufa siku yoyote na wala halitadumu kabisa.
Akiongea katika kipindi cha eNews, Moni anasema kuwa kwa sasa amekuwa akimshangaa msanii mwenzie huyo Nikki Mbishi kwa kuwa muda wote amekuwa ni mtu wa kulalamika tu kuhusu wasanii wenzake huku kazi zake hata hazionekani kufanyika.
Moni anasema kuwa yeye na msanii mwenzake wanafanya rap kama biashara na wala sio kama ambavyo Nikki Mbishi amekuwa akitaka kuifananisha na kazi za kilingeni na wala maneno ya msanii mwenzao huyo hayawezi kuwafanya waache kazi zao.
Moni anasema kuwa kinachomfanya Nikki Mbishi asumbuke na kuongea maneno juu ya kundi lao ni ule uzoefu wa wasanii wengi kuona magroup kuwa yanavunjika kila mara bila kujua kuwa kuvunjika kwa group utokana na uzembe wa wasanii wenyewe.