Nikija Kwenye Mazingira ya Harusi Napata ka Moyo Ka Na Mimi Pia:-Ben Pol
Msanii wa muziki wa RnB Ben pol amefunguka na kusema kuwa kwa muda sasa amekuwa akihudhuria harusi za wasanii wenzake na yeye anapata moyo wa kutamani kufunga ndoa kama wenzake na anaamini kuwa Mungu ni mwema na yeye atakamilisha ndoa yake hivi karibuni.
Alikuwa akiyaongea hayo siku ya harusi ya msanii mwenzao stamina ambapo wasanii kadhaa akwepo Ben Pol, Young Killer pamoja na roa waliamua kufanya kitu cha tofauti katika uande wa burudani kwa kuhudhuriwa wao wenywe na kufanya shughuli hiyo .
Akiongea na cloud tv, Ben Pol nasema kuwa amekuwa akipata moyo wa kuoa mara kwa mara na anaona kabia zamu yake imefika ili pia watu waweze kuja kwake na kusherekea kama vile ambavyo yeye amekuwa akienda kufanya hivyo kwa wenzake na anaamini kuwa yatatimia .
Stamina na mpenzi wake wa siku nyingi walifunga ndoa wikiendi hii na ndoa hiyo kusimamamiwa na msanii Roma ana mke wake huko mkoani Morogoro.Tunawatakia kila lenye kheri wanaharusi hawa wapya lakini pia wasanii wengine waweze kuiga mfano mzuri kutoka kwa wasanii wanaoamua kufunga ndoa na sio kuishia njiani katika mahuiano.