Ney Wa Mitego aongelea bifu za wasanii
Kumekuwepo na bifu nyingi sana zinazoendelea katika mitandao dhidi ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movies, kwa ujumla katika tasnia ya sanaa ,bifu hizo zimekuwa zikiibuka bila kujali ukongwe au upya wa wasanii wanaojiingiza katika bifu hizo, huku baadhi ya sababu za mifarakano hiyo kutokujulikana kwa uhalisia wake, kuna baadhi wanaogombana kwa sababu ya wivu, wapo wanaogombana tu ili kupata kiki katika tasnia , ila wapo wanaofanya hivyo ili kukuza game la kazi zao.Kwa kiasi kikubwa katika tasnia, Bongo Fleva imekuwa ikiongoza katika kuzusha bifu baina yao ,huku wengine wakiingia hadi studio kuandika wimbo kwa ajili ya kujibu yale wanayotuhumiwa na wasanii wenzao.
Msanii wa Bongo Fleva Emmanuel Elbariki Munisi maarufu kama Ney Wa Mitego “True boy” anaetamba kwa sasa na kibao chake kipya cha “maku” , lakini pia ni moja ya wasanii ambao hujikuta matatani na wasanii wenzie kwa sababu ya nyimbo nyingi anazotoa huku akitoa madongo kwa baadhi ya wasanii au yanayotokea katika jamii kwa ujumla.
Ney Wa Mitego anasema kuwa anaposikia wasanii wana bifu huwa anawaza vitu viwili ‘huwa nawaza chachu kwenye game kati ya bifu yao, pia nawaza biashara wanayoenda kuifanya ” hivyo uwa anaangalia je ilo bifu yupo nani na nani na akishaajua uwa anafanya tathmini ya bifu ilo kama kama itakuwa ni biashara nzuri au la. Ney anasema kuwa endapo atagundua kuwa bifu ilo sio la kibiashara au linatoka moyoni basi kwake bifu ilo huwa sio zuri.”Game zuri ni lile linaloleta challenge katika muziki ,tuwe na ushindani wa kutoa nyimbo nzuri, au tuwe na ushindani wa kujaza watu kwenye show”Aliongezea Ney.
Ney Wa Mitego anaongezea kuwa bifu litakuwa zuri kama unasikia mtu katoa ngoma na wewe unatoa ngoma, msanii huyu kanunua gari na wewe unanunua nyumba, wasanii wawe na bifu la kuwaasha mashabiki, lakini kama bifu ilo litakuwa lenye kuleta chuki na kinyogo inayoanzia moyoni huwa sizisapoti na sizipendagi.