Ney Wa Mitego Amekuja Na nguvu Ya Kitaa
Msanii wa bongo fleva Ney wa Mitego amekuwa mbunifu na kuja na tour ya muziki inayojulikana kama nguvu ya kitaa ambayo itajikita kusabahi mashabiki wote waliopo kitaani, kwa sababu wanaami kuwa mtaani ndipo mashabiki wanaowapa viburi katika kazi wanapatikana.
Akiongea katika kipindi cha Siz wa kitaa cha Clouds Tv, msanii Ney wa Mitego alisema kuwa ziara hiyo inayojulikana kama nguvu ya kitaa imekuwa na lengo la kuwafikia mashabiki wote wanaopatikana mitaani tena hasa uko uchochoroni kwa sababu anachoamini yeye ni kuwa wanaosapoti na kupenda muziki wao ni watu kutoka katika mitaa tu na wala sio watu matajiri kama watu wanavyofikiria
Tumeamua kurudisha fadhila kwa mashabiki wetu ambao wanapatikana mitaani, watoto wa mitaani kama tandale, masaki na sehemu za watu wa chini ndio wanaosapoti muziki wetu na wala sio watoto wa kishua, hata hivyo ukiangalia wasanii wengi wa muziki tumetokea huko kwenye maisha magumu wala sio maisha mazuri hivyo ni bora kuwa kumbuka wenzetu wa hali ya chini ambao wanatupa jeuri ya kuafnya kazi mjini
Hata hivyo akiendelea kuoingezea anasema kuwa shoo iyo itakuwa inagharimu kiasi kidogo cha shilingi elfu tatu tu kila sehemu na itaanza asubuhi ya saa nne mpaka pale watapoona mashabiki wao wametosheka na muziki wao.
Hata hivo, Ney wa Mitego anaendelea kusema kuwa katika mitaa yao kuna shida nyingi za kijamii hivyo fedha zitakazokuwa zinapatikana zitakuwa ni kwa ajili ya kusaidia sehemu hizo, kama hospitali na vituo vya watoto yatima na wafanyabiashara ndogondogo watakaokuwa wanakutana nao mitaani.Akitolea mfano anasema kuwa hata yeye alishaenda kwenye hospitali moja na kutoa kidogo alichokuwa nacho ili kusaidia hospitalini hapo.
Tamasha hilo ambalo limeanza jumamosi ya tarehe 04, katika viwanja vya Tanganyika Peakers linategemea kuendelea kwa baadhi ya mikoa ili kuwafikia mashabiki wanaopatikana katika mitaa na ambao hawaezi kwenda kwenye viwanja vya starehe kwa gharama kubwa ili kuwaona wasanii wao kwa bei ndogo.