Nelly Kamwelu Yupo Njiani Kufunga Ndoa
Mlimbwenda ambaye amewahi kushikilia mataji mbali mbali ya urembo hapa nchini ikiwemo Miss Universe Tanzania, Nelly Kamwelu amesema yupo njiani kuolewa.
Nelly amefunguka na kuweka wazi kuwa mwanaume anayetarajia kumuoa hivi karibuni sio mtu maarufu lakini ni mwanaume ambaye amekuwa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Nelly alisema kuwa anamshukuru Mungu ameweza kumpata mtu ambaye anampenda na anaahidi kuwa mke bora baada ya tukio hilo la heri kukamilika.
Unajua kila jambo na wakati wake, yamesemwa mengi juu yangu lakini nashukuru Mungu siku si nyingi nitaandika historia katika maisha yangu, kwa lugha nyingine ni kwamba naolewa ‘soon’ kwani nimeshachumbiwa”.