Ndoa Ya Irene Na Ndikumana Haijavunjika
Baada ya kusambaa kwa picha nyingi za harusi kati ya msanii wa bongo fleva Dogo Janja na msanii wa bongo movie , mwanadaada mlimbwende katika tasnia hiyo Irene Uwoya na hata baadae watu hao kuamua kuthibitisha ndoa iyo ingawa baadhi ya mashabiki na watu wao wa karibu bado wakiona ni kama kitendawili kilichokosa majibu kwa wawili hao kuoana.
Hata baada ya kusambaa kwa picha hizo , mume wa kwanza wa Irene Uwoya anaefahamika kama Ndikumana ambae walifunga nae ndoa ya kikristo kanisani pia alijibu mapigo kwa kuweka post akiwa na mwanamke mwingine inaesemekana kuwa ni wa nchini kwao.Wawili hao walitengena bila idhini ya imani yao iliyowaunganisha kukubali wao kutengana .
Akizungumza na moja ya waandishi wa habari wa gazeti pendwa hapa nchini moja ya waasisi wa dini ya kikristo ambae hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa hata kama Irene Uwoya ameamua kuolewa na mwanaume mwingine lakini bado ndoa yake na mumuwe wa kwanza aliefunga nae kanisani bado inatambulika palepale kwa sababu kanisa lilichukua jukumu la kuwaunganisha kwa makubaliano na pia ilitakiwa warudi tena kanisani kupata ushuruhishi wa matatizo yao.
Ndoa yao bado ipo hai kabisa kanisani kwa sababu kanisani kwetu hauna talaka,talaka itatoka pale kumegundulika tatizo kubwa kama mmoja atakuwa anazini na ushahidi ukawepo kabisa au kutokee tatizo la kinyumba ambalo haliwezi kutatulika ndio kibali cha talaka kitatolewa na ndoa itabatilishwa lakini kimsingi kabisa kanisa halitambui talaka.
Hata hivyo kiongozi huyo alisema kuwa kwa kile anachokifanya Irene na muwe wake huyo wa ndoa kwa kubadilsha wanawake kila siku ni dhambi ya kizini ambayo kanisa pi inaikataza.
Kanisa linakataza kabisa uzinzi na wanachokifanya wao kwa sasa ni uzinzi,kitendo hicho hakimpendezi mungu kabisa, kwa sababu ni kinyume na biblia inavyosema na imani ya kikristo.wanatakiwa wabadilike wakae wamalize tofauti zao.
Irene Uwoya na Ndikumana walifanikwa kufunga ndoa na kuzaa mtoto mmoja ambae , kwa sasa Irene ameolewa ndoa ya kiislamu na kuachana na ndoa ya kikristo aliyokuwa nao kwanza.