Navy Kenzo Watangaza Ndoa hivi Karibuni.
Wasanii wa zamani wanaounda kundi la Navy kenzo Aika na Nahreel wametangaza ndoa yao inayotarajiwa kufungwa hivi karibuni huku ndoa iyo ikionekana kutarajiwa kufanyika huko kijijini kwao moshi,
Katika ukurasa wa instagram wa nahreel aliweka picha inayowaonyesha wakiwa Egypt wakisherekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa na Nahreel huku wakiandika kuwa ndoa coming soon na kufuatiwa na comments za wasanii mbalimbali akiwepo vannesa mdee.
Katika picha hiyo aliandika ” more life, more love , love you @aikanavykenzo soon wedding... ”
Hata baada ya maneno hayo wasanii walianza kuwapongeza na kuwatakia kheri katika maamuzi hayo wanayotaka kuyachukua.
Kwa zaidi ya miaka kumi wawili hao wamekuwa pamona na kufanikiwa kupata mtoto mmoja anaitwa GOLD