Navy Kenzo Waibuka Kidedea Katika Tuzo za Soundcity
Wasanii wa muziki wa Bongo fleva wanaounda Kundi la Navy kenzo, Nahreel na Aikah Marealle wameonekana kidedea katika tuzo za Soundcity Awards za nchini Nigeria.
Navy kenzo walikuwa moja kati wasanii sita waliotajwa kutoka Tanzania na ndio waliofanikiwa kupata tuzo ambapo wameshinda kipengele cha Best Group or Duo.
https://www.instagram.com/p/BsSlddNASqp/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=kbwrq7qnvxfc
Wasanii wengine waliochaguliwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Diamond Platnumz, Mbosso, Lava Lava na Harmonize kutoka WCB Lakini pia Maua Sama na Navy Kenzo.
Katika tuzo hizo Msanii Burna Boy ameshinda tuzo hizo kwenye vipengele vya Msanii Bora wa kiume Afrika, Wimbo bora wa mwaka (YE), Listeners Choice Awards na Best Male MVP.
Kwenye vipengele hivyo vyote alivyoshinda, alikuwa anapambana na wasanii wakubwa kama Diamond, Wizkid, Davido, AKA, Cassper Nyovest na wengineo.