Natasha Afungukia Kauli Ya Kanumba Inayomtesa Mpaka Leo
Muigizaji mkongwe wa Bongo movie mwanamama Suzan Lewis maarufu kama Natasha amefunguka kuhusu mambo mengi katika sanaa ya Bongo movie akiwemo kumuongelea Marehemu Steven Kanumba.
Katika interview yake na gazeti la Amani, Natasha aliulizwa kuhusu Marehemu Kanumba ambaye ameshawahi kufanya naye kazi kadhaa ambapo ameweka wazi kuwa alikuwa mtu mzuri sana na mwenye upekee;
Kiukweli Kanumba alikuwa ni bosi wangu lakini alikuwa ni mwenye heshima sana, alikuwa anakusikiliza nini unataka, na alikuwa siyo mtu wa kujisikia na pia kwenye malipo alikuwa ananilipa vizuri tofauti na wengine huwa wanaleta kujuana sana”.
Lakini pia Natasha alipoulizwa anakumbuka nini kuhusu Kanumba alifunguka na kutaja kauli yake ya mwisho kwake miaka kadhaa iliyopita;
Kitu ambacho sitaweza kumsahau kuna siku tulikutana naye nilikuwa mimi na Monalisa tulikuwa tunaenda kanisani, akasimamisha gari tukasalimiana akasema; “Hee! Ndio mnaenda kwenye lile kanisa lenu?” Nikamjibu; ‘ndio’, akasema; “He! Hilo kanisa lenu mnasali mpaka mnamboa Mungu, mnasali asubuhi mpaka jioni!” yaani ile kauli mimi huwa inaniuma sana kila ninapoikumbuka”.