Natamani Sana Kuimba Nyimbo za Gospel-Maua Sama

Mwanadada anaetamba sasa hivi na kibao chake cha Nakuelewa Maua Sama amefunguka na kusema kuwa anatamani sana kuimba nyimbo za gospo kwa sababu mara nyingi amekuwa akijikuta akizisikia au kuimba anakuwa na raha sana.

Maua Sama ambae alitambulika zaidi  na wimbo wake wa mahaba niue , amesema kuwa kila siku amekuwa anatamani sana kuimba nyimbo za kuhamasisha jamii na kwa jinsi anavyoona anatamani sana siku moja kuimba nyimbo za gospo na anahisi ipo siku ataimba tu kwa sababu ndicho kitu anachopenda pamoja na kwamba mwanadada huyo ni muislamu.

download latest music    

Napenda sana nyimbo za Inspiration,kuna wakati nafikiriaa natamani  na  ninajikuta nataka  kuimba sana nyimbo za gospo,ipo siku nitaimba kwa sababu ni kitu nimekuwa ninakipenda sana kutoka moyoni.-Alifunguka Maua sana.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.