“Natamani Kuzaa” Elizabeth Michael ‘Lulu’ afunguka kuhusu kuwa mama
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni mmoja wa wanawake maarufu Tanzania kwa sababu ya sinema za Kibongo. Hata hivyo wenzake wamekuwa wakizaa na kulingana na mahojiano yake na 4-Tamu pia yeye anatamani mtoto.
Hii ni mara ya kwanza kwa Lulu kusema haya. Katika mahojiano yake Lulu alisema kuwa imefika wakati na yeye anatamani sasa kuzaa.
Aliendelea kusema kuwa umri wake unamruhusu na akipata mwanaume wa kumzalia basi atajaribu kupata mtoto. Akizungumza na 4-Tamu alisema;
“Natamani tu na mimi nipate mtoto sema ndiyo hivyo bado natengeneza mipango ya mimi kuwa mama tena mama bora,”