Nampenda Sana Tanasha – Esma Platnumz
Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka na kudai kuwa anamkubali sana wifi yake mpya Tanasha kwa muda mfupi ambao amemjua.
Esma ambaye amekutana rasmi na Tanasha siku chache zilizopita amedai kuwa ameshaanza kumpenda ‘kumoyo’ wifi yake mpya Tanasha Donna kiasi cha kujiuliza kwamba, mwanadada huyo alikuwa wapi siku zote hizo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda Esma alisema amekuwa na ukaribu kwa muda mfupi na wifi yake huyo lakini ametokea kumkubali na sasa amekaa kwenye moyo wake tofauti na alivyotarajia mwanzo kwani mtu akiwa mpya kumzoea inahitaji moyo kuridhia.
Huwezi amini Tanasha tayari ameshakaa ndani ya moyo wangu, nampenda sana na kuna muda najiuliza alikuwa wapi muda wote? Kwa nini hakutokea mapema kwenye familia yetu? Hayo mambo ya kuniita Yuda hata siyajali kabisa, watajua wenyewe kwani mimi maisha yanasonga”.
Diamond alimtambulisha Tanasha kwa Familia yake aliweka mama yake mzazi Mama Dangote siku chache zilizopita.