Namkubali Sana Jay Dee Kuliko Msanii Mwingine:-Lady Jay Dee
Msaniii mkongwe wa muziki nchini ambae alipata cheo cha kuwa dada mkuu katika muziki wa bongo lady jay dee amefunguka na kudai kuwa katika kazi zake za muziki msanii anaemkubali kupita wote ni yeye mwenyewe na anawaheshimu sana baadhi ya wasaniii wakubwa na wakongwe nchi.
Lady Jay Dee ambae ana haki ya kusema hayo kutokana na magumu mengi ya muziki aliyopitia mpaka sasa pamoja na changamoto za kuwa na wasanii wengi wa kike chipukizi lakini bado yupo katika game na anasimama vizuri anasema kuwa wasanii wengi wanafanya vizuri lakini kwake kuwa anajikubali mwenyewe zaidi kuliko mtu yoyote.
Namkubali sana lady jay dee kuliko wasanii wengine wote wa kike tanzania.ila pia ninawaheshimu sana Khadija Kopa na Patricia Hillary.
Mwandishi pia alipata bahati ya kumuuliza Jay Dee kuhusu tetesi zake za kukaa nje ya Tanzania na kuhamishia makazi yake nchini nigeria ambapo yupo mpenzi wake Spicy Music na hata kufanya kazi zake huko , lakini jJay Dee alisema kuwa Tanzania ndio nyumban, nigeria atakuwa anakwenda na kurudi tu kwa kuwa kila kitu chake alitengeneza hapa.
Kwenda na kurudi sawa lakini sio kuishi moja kwa moja huko,kwa aslimia kubwa sana maisha yangu yote nimeyajenga Tanzania, ila inawezekana ikibidi,
Mpaka sasa Jay Dee anaweza kuwa ndio msanii mkubwa wa kwanza wa kike mwenye album nyingi sana tanzania pamoja na kwamba jwa sasa wasanii wameanza kuwa na msimamo wa kutoa album lakini bado jay dee anaongoza kwa hilo.