Najuta Kupoteza Miaka 6 Kwa Ajili ya Makomandoo-Muki
Baada ya habari kusambaa kuwa kundi la muziki la Makomandoo limesambaratika habari amabzo ziliwekwa wazi na Fredy Whine ambae ni mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, na kusema kuwa kwa sasa kundi hilo limekufa kwa sababu mwenzake Muki yuko busy na familia na kwamba familia yake inambana sana kufikia hatu akushindwa kufanya kazi.
Lakini baada ya taarifa hizo kusambaa , Muki pia ameamua kufunguka na kusema kuwa sio kweli kuwa familia imemfanya yeye na Fredy waachana na washindwe kufanya kazi za muziki.Hata hivyo Muki amesema kuwa alishangaa sana kuona habari kama hizo kwenye vyombo vya habari na hata ndugu zake walitaka kujua kama wamegombana.
Alitaka kunipeleka polisi kisa gari,tukafanya nyimbo lakini nikawa nasikia anafuta sauti zangu,Nilimwambia kuwa nimeshachoka na isiwe shida itafika sehemu mimi nitaamua maamuzi magumu lakini kabla ya mimi kuamua nashukuru kaanza kuamua mwenzangu.
Ilo ni tatizo lingine ambalo ananitangazia kuhusu familia, kwamba inafanya nisifanye muziki lakini hata yeye ana familia pia na familia yake haijali kabisa, na ndio maana anaona mimi nimebanwa na familia , hakuna ukweli huo.
Baada ya kuongea hayo yote , Muki alisema kuwa sababu kubwa ya wao kugombana ni kwa sababu msanii mwenzake huyo ana roho mbaya hivyo hawawezi kukaa wote na kufanya kazi.
Tatizo kubwa la ndugu yangu yule ana roho mbaya,mpaka mimi mwenyewe uwa namwambiaga kuwa wewe sidhani kama kwa roho yako hiyo tutaweza kufanikiwa kwa sababu mimi naona kabisa ambavyo mimi ninavyoshow love kwako.