“Naanzaje Labda Kutembea na Shetta”- Lynn
Videi vixen ambaye Hivi karibuni aligeukia gani ya Bongo fleva, Irene Godfrey maarufu kama Official Lynn amefunguka na kudai hawezi hata siku moja kutembea na msanii mwenzake Nurdin Bilal ‘Shetta.
Lynn amesemameweka hayo Baada ya tetesi zilizowahi kusambaaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa wawili hao ni wapenzi kutokana na ukaribu ambao wamekuwa nao sasa.
Katika mahojiano yake na Gazeti la Risasi Jumamosi, Lyyn alisema kuwa ukaribu wake na Shetta unatokana na kazi wanayoifanya kwa pamoja lakini alishangazwa na maneno kwamba wanatoka kimapenzi kitu ambacho siyo kweli.
Hivi naanzaje kutoka na Shetta jamani kwa hiyo kila mtu nitakayekuwa naye karibu ni bwana wangu? Shetta ni mshikaji wangu, siwezi kutoka naye na huku Afrika Kusini tumekuja kikazi wala siyo kula bata kama watu wanavyosema ila kwa kuwa wanapenda kutunga uongo waendelee tu kuamini, sina muda wa kuwalazimisha waelewe, napiga kazi tu”.