Mzee Zahiri Zorro Aongelea Kifo cha Mwanafunzi Akwilina
Mwanamuziki mkongwe na tasnia ya muziki nchin Mzee Zahiri Ally Zorro ambae pia ndio baba mzazi wa msanii Banana Zorro na Maunda Zorro ameongelea kusikitishwa kwake na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini ambae alipigwa risasi wiki iliyopita na inaosemekana kuwa ni maaskari ambao walikuwa katika doria la kutuliza ghasia na maandamano ya wafuasi wa chadema katika uchaguzi mdogo Kinondoni jijini Dar.
Mzee zorro anasema kuwa yeye anaiamini sana serikali iliyopo madaraani hivyo anachoamini ni kuwa yeyote alifanikisha kifo cha mwanafuzni huyo pia serikali itafanikiwa kumpata na kumpa hukumu anayostahili kupewa kwa kosa hilo.Hata hivyo Zzee zorro ameipongeza sana serikali kwa kujitoa kwa moyo wote kugharamikia mazishi ya binti huyo ambae wazazi wake ndio walikuwa tumaini lao.
Asante wa serikali yetu sikivu sana,kusikia kilio cha wngi na kujitoa kumrudisha akwilina nyumbani, vifo ndio hutokea kwa wakati na muda uliopangwa japo sababu za vifo huwa ni tatanishi.tunaamini kuwa mkono wa serikali hii ni mrefu utafanikisha kukamatwa kwa muuaji na ni vyema akamatwe ili asije kuua tena.
Akwilina ambae alikuwa ni mwanafuzni wa mwaka wa kwanza katika chuo cha usafirishaji cha NIT jijini Dar, aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani alipokuwa katika daladala akitokea Bagamoyo ambako alikwenda kwa ajili ya kupeleka barua ya maombi ya mafunzo kwa vitendo.
Kifo cha mwanafunzi Akwilina , kimekuwa ni moja ya vifo vilivyowahi kutokea Tanzania na kuwaumiza watu wengi kutokana na ukweli kwamba haukuwa imepangwa na hakuna aliyetgema kuwa kutatokea tukio kama ili linalohusishwa na matendo ya uchaguzi.