Mzee Majuto Atembelewa na Mh.Rais Hospitalini.
Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini , Mzee Majuto amaetembelewa na Mh .Raisi Magufuli hospitalini alipokuwa amelazwa mpaka sasa ambapo bado anapokea matibabu ya ugonjwa wa tezi dume aligundulika kuwa nao siku kadhaa zilizopita.
Mzee Majuto ameonyeshwa kufurahishwa na ujio wa Raisi na kumpongeza kwa kazi yake nzuri anayoifanya sasa ya kuwafanya wananchi wote kuwa na moyo wa kufanya kazi na kujituma , lakini pia amesifia na kusema kuwa uongozi wa Raisi huyo umekuwa wenye baraka na neema kwa sasa sasa hivi nchi iko vizuri kwa kila mtu,
Akiendelea kuongea baada ya Mh.Raisi kutoka hospitalini hapo, Mzee Majuto anasema kuwa yeye ndie alikuwa mtu wa kwanza kutabiri kuwa Magufuli angeweza kushinda uraisi na angeweza kuiendesha nchi na ndicho anachokifanya sasa.
mii ndie mtu wa kwanza kutabiri kuwa akiwa raisi itakuwa shughuli hapa,nilishukuru kuchaguliwa kwa huyu bwana, hapa tumepata raisi sio masihara hasa, watu wote sasa wana adabu zao.wanajua nini maana ya kazi na akisema tu jambo watu wanatekeleza haraka sana.
wezi wanakamatwa, wala rushwa wanakamatwa, na wenye vyeti feki hata kama ulifanya kazi miaka 20 iliyopita fukuza, hii safi sana.
Sisi wazee tunafarijika sana, hivi viwanda sasa hivi vinatapakaa kila sehemu na leo hamekuja kunitembelea hospitali siujui kama kuna watu hawajajikojolea hapa kwa uoga maana hataki masihara kabisa.hii ndio raha ya kupata kiongozi bora mwenye msimamo.
Pamoja na kumpongeza lakini pia Mzee Majuto anasema kuwa sio kazi rahisi kwa wananchi kupata kiongozi mzuri kama Magufuli hivyo waweze kumtumia vizuri.
Mzee Majuto amelazwa katika hospitali ya Tumaini iliyopo jijini Dar wiki iliyopita baada ya kutolewa nyumbani kwake Tanga na kuletwa huku kwa matibabu zaidi na kukutwa na tezi dume , na mpka sasa bado yuko hospitali kwa kuendelea na matibabu.
Mh.Raisi alipokutana na Mzee Majuto akiwa hospitalini.