Mzee Majuto Akimbizwa Hospitali Baada ya Kuzidiwa Ghafa.
Mwigizaji wa maigizo ya vichekesho na filamu nchini, Mzee Majuto amekimbizwa hospitali baada ya hali yake kubadilika ghafa na kuzidiwa .mzee majuto ambae amekimbizwa hospitali ya tumaini jijini dar ambapo alikuwa akipatiwa matibabu tangu mara ya kwanza amepelekwa hospitali hapo kwa ajili ya kuangaliwa tena afya yake.
Ikumbukwe kuwa Mzee Majuto aliwahi kuuumwa mara ya kwanza na kuthibitisha kuwa alikuwa akisumbuliwa na tezi dume hivyo alifanyiwa uapsuaji kwa ajili ya kutibu mardhi hayo lakini hali yake baada ya kubadilika inasemekana kuwa kidonda chake kimekuwa kikimsumbua kwa muda mrefu hivyo kinashindikana kupona na kusababibisha kutoka maji.
Akiongea na waandishi wa habari, mke wa Mzee mMajuto amesema uwa ni kweli mume wake amepeleka hospitali baada ya hali kubadilika na kukimbizwa hospitali huku akisema kuwa tatizo kubwa ni kidonda alichofanyiwa upasuaji kushindwa kupona na kutoa maji.