Mzee Abdul:Zari na Hamisa Wote Wana Haki Sawa

Baba mzazi wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kuongelea bifu kali linaloendelea kati ya wanawake wawili Zari na Hamisa ambao ni wazazi wenza wa mtoto wake huyo wa kiume na kusema kuwa wanawake hao wote wawili hawapaswi kuwa wanagombana kwa sababu wote wana haki sawa kwa sababu hakuna alieolewa na msanii huyo.

Akiongea na gazeti la amani juzi kati baba huyo amesema kuwa kitendo cha wanawake hao kuwa wanavuana nguo katika mitandao ya kijamii limekuwa likimkwaza sana kwa sababu wote wana haki sawa tu.

download latest music    

Ninawasihi hawa wana wake waache malumbano katika mitandao ya kijamii,kwa sababu kila mmoja amzaa kwaio kila mmoja  wana nafasi moja na haki sawa kwa sababu hakuna aliyeolewa mpaka sasa.maneno wanayotoleana katika mitandao ya kijamii yanakwaza na kuchukiza mno sasa naomba niwaase wanakuwa kuwa wote wao wana haki sawa tu,, mwanangu bado hajaoa na inawezekana mmoja akaolewa lakini mwingine akapewa heshima yake yu kama mzazi wa mtoto wake, lakini pia wote wanaweza kuolewa kwa sababu dini ya mwanangu inaruhusu.

Mzee abdul anasema kuwa wanwake hao wanyamaze mpaka mtoto wake huyo wa kiume atakapoamua kutoa uamuzi wa kuoa.

Kitu ambacho nina uhakika nacho ni kuwa kwa sababu kila mmoja kazaa na mwanangu basi kila mmoja ataambulia chochote kitu.

Hata hivyo mze huyo mara ya kwanza alikuwa akionekana kuwa yupo upande wa hamisa mobeto na hata kug=hudhuria party ya mtoto wa Hamisa Mobeto na Diamond Platinumz siku za nyuma.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kulizuka kwa tetesi kuwa mwaka huu 2018 inaweza kufanyika harusi kubwa na yenye gharama ya msanii diamond na mzazi mwenzie Zari , hii ikiwa na maana kuwa tayari mke wa kuoa alishapatikana.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.