Mwenyekiti Uvccm Hamtambui Wema, Agoma Kuzungumza Kung’olewa kwa Jokate
Mwenyekiti wa UVCCM kheri james amefunguka na kuzungumzia nafasi ya jokate na wema sepetu katika umoja huo wa vijana wa ccm.akizungumza katika kipindi cha kikaangoni live kinachorushwa na EATV. mwenyekiti huyo amesema kuwa hawezi kuzungumzia swala lolote kuhusu kuondolewa kwa jokate katika nafasi hiyo kwa sababu wakati wanamueweka hawakuzungumzia katika media.
“Kama ambavyo hatukuweza kuweka wazi kuhusu kuteuliwa kwake Jokate, ndivyo ambavyo hatuwezi kuzungumzia kutolewa kwake,
Kuhusu Wema kwakweli Wema mimi simjui,namsoma tu kwenye magazeti kuwa amerudi CCM na sio UVCCM”
March 25 mwaka huu kamatiya UVCCM ilitengua uteuzi wa kaimu katibu wa UVCCM ambae ni jokate mwegelo bila kutoa wazi sababu za kutengeliwa kwake na pia mapema Decemba mwaka 2017 wema alitangaza rasmi kurudi CCM alikokuwa kabla ya kwenda CHADEMA hapo awali.