Mwarabu Fighter Afunguka na Kueleza Alivyoteseka Kufanya Kazi Kwa Diamond
Bodyguard aliyejizolea umaarufu Bongo baada ya kufanya kazi kwa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter amefunguka na kuanika magumu aliyopitia kufanya kazi kwa Diamond.
Katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa Bongo 5, Mwarabu Fighter amefunguka na kuanika mazingira magumu aliyopitia wakati anafanya kazi kwa staa huyo:
Nilikuwa nakatwa mshahara nikichelewa kwenye tukio siku unaenda kupokea mshahara unakuta hata laki na nusu hakuna halafu unakutana na kijikaratasi kikieleza na kukupa ufafanuzi kuwa siku fulani ulichelewa pia unakumbuka siku fulani?”.
Lakini pia Mwarabu Fighter ameweka wazi kuwa kuna baadhi ya siku za mapumziko alizokuwa anatakiwa apumzike nyumbani alikuwa anapigiwa simu aende kazini na kupewa dakika kumi au kumi na tano.
Mwarabu Fighter ameweka wazi kuwa wakati anafanya kazi kwa Diamond aliishia kupata ajali ya pikipiki mara nne katika harakati za kuwahi kazini.