Mwakifamba Alalamikia Kitendo cha Wastara Kuomba Msaada.
Raisi wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba amelalalmika kitendo cha msanii wa kike Wastara Juma kuomba msaada katika vyombo vya habari na kwa viongozi na kulalamika kuwa hapatiwi msaada wowote ilhali hakuwahi kusema taarifa hizo kwa uongozi wake tangu alipogundua kuwa hawezi kusiamama peke yake bila kupatiwa msaada.
Mwakifamba anasema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakijua Wastara ni mgonjwa na anaendelea na matibabu lakini taarifa za sasa kuwa anahitajika kwenda India na hana ela kwa ajili ya matibabu hazijawafikia viongozi hao rasmi kwaio wameshindwa kujua zaidi ya kuona katika mitandao kama wasanii wengine wanavyoona katika mitandao tu.
Raisi huyo amesema kuwa kitendo alichokifanya wastara sio kizurikwa sababu hata mara ya kwanza alipopata matatizo uongozi wa shirikisho la filamu lilikuwa ni moja ya watu wa mstari wa mbele kabisa katika kuwasaidia ili aweze kapata matibabu.
Hivi karibuni wastara alifunguka katika mitandao ya kijamii na kuomba watu wamsaidie ili aweze kupata ela ya matibabu yake ya mguu ambao kwa sasa umefikia katika hatua mbaya na kwamba anapata maumivu makali sana katika mgongo wake kutokana na kushindwa kurudi kliniki kwa matibabu.
Wastara ambae alipata ajali ya gari miaka kadhaa iliyopita na kusababisha kukatwa mguu wake na kuwekewa mguu wa bandia alitakiwa kurudi hospiatali siku nyingi zikiwa zilishapita lakini alishindwa kufanikisha ilo kutokana na kukosekana kwa fedha, hii imemsababishia maumivu makali ya mgongo yanayompelekea muda mwingine hata kuzimia.