Mwaka 2019 Lazima Niolewe Nimechoka Kusubiri- Tiko
Muigizaji wa Bongo movie na msanii wa Bongo fleva Tiko Hassan ameibuka na kuweka wazi nia yake kutaka kutafuta mume na kuolewa kwa mwaka huu wa 2019.
Tiko amefunguka na kusema yeye Kama mwanamke ambaye anajiamini kuwa amekamilika anatamani sana apate mwanaume wa kuwa mwenza wake kwani amechoka kusubiri.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Tiko alisema kuwa ndoa ni heshima kwa kila mwanamke na amesubiri kwa muda mrefu bila mafanikio lakini imani yake ni kwamba, atauona mwaka wa 2020 akiwa ni mke wa mtu.
Jamani nimechoka kusubiri lakini naamini mwaka huu utakuwa ni mzuri kwangu, kila kwenye ibada namuomba Mungu anijaalie mume bora ndani ya mwaka huu“.
Lakini pia Tiko ameweka waiz anataka mwanaume ambaye atakuwa na utayari wa kumuelewa kutokana na kazi anayofanya.