Muziki Wangu Nauheshimu,Sijichukulii Poa:Country Boy.
Msanii wa muziki wa hip-hop nchi Country Boy anasema kuwa ukiwa msanii ni lazima kuwe na mipaka ya ufanyaji kazi ili muziki wako uweze kufanya vizuri na kama wewe mwenyewe hautajiheshimu hakuna atakae heshimu muziki wako na kuuogopa.
Country Boy anasema kuwa kuna wasani wengi sana wamekuwa wanashindwa kumfuata kwa ajili ya kufanya nae kazi kwa sababu alishatengeneza kuogopwa kwa muziki wake ili uwe na thamani kila siku.
Ukiwa msanii ni lazima uwe na value yako sio unakuwa mtu wa kawaida tu ,na hiyo ndio biashara siku zote.ninavyojiweka na mazingira yangu ndio yanayonifanya nazidi kuogopeka siku zote hizo katika muziki wangu na hiyo ndo inanifanya naogopeka kiasi kwamba ukija lazima uje na muziki mzuri tu.
hata mimi mwenyewe muziki wangu nauchukulia serious zaidi,kila ninachokifanya ni lazima nikiogope zaidi na nikiheshimu, sijawahi kujichukulia poa.-Alifunguka msanii huyo.