Muna Kufuta Tatoo Kwa Zaidi ya Milioni Tano.
Mwanadada mjasilimali na muigizaji Rose Alphonce amefunguka na kudai kuwa atatumia zaidi ya milioni tano kufuta tatoo zilizopo mwilini mwake , Muna ambae alisema kuwa kwa sasa ameokoka hivyo tatoo hizo zimekuwa zikimnyima amani sana anatamani kuzifuta tatoo hizo na anaona kabisa kuwa ni lazima azifute.
Muna anasema kuwa mpaka sasa hivi ana michoro kama mitano mwilini mwake huku tatoo iliyopo shingoni ndio kubwa kuliko zote lakini alishafanya mpango wa kuuliza sehemu ambayo angeweza kufuta tatoo hizo na kuambiwa kuwa inawezekana kufutwa kwa milioni tano.
Tayari nimeshaulizia kwa wataalamu huko thailand,ambao watanifuta bila kupata madhara yoyote na wameniambia kuwa hizo zingine ndogondogo zitakuwa ni chini ya milion 2.1.