Muna Afungua Patrick Foundation ya Mwanae.
Mwanadada Muna love amefanikiwa kufungua Foundation yake itakayo itwa Patrick Foundation ambayo itakuwa na kazi ya kusaidia watoto wenye matatizo mbalimbali katika jamii huku lengo kubwa ikiwa ni kwa ajili ya kuwasaidia na pia kumkumbuka mtoto wake.
Muna amekuwa akiguswa sana na kutokuwepo kwa mtoto wake huyo ambae alifariki mwaka huu, hivyo Muna aliamua kufanya hivyo kama kuguswa na watoto wanaoteseka mitaani .
Dhumuni la muna inadhihirika sana pale aliapoanza kutembea mikoa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto hao waliopo mitaani na wale walio wagonjwa ambao wamekuwa wakikosa misaada ya kiafya na pia kielimu.