Mtoto Mwingine Kuletwa Madale, Yasemekana Ni Mchepuko Wa Diamond
Siku chache zilizopita ambapo mwanamama Zari The Bossy aliezaa na Diamond Platinumz kuwasili nchini kwa ajili ya kuja kusherekea pamoja harusi ya Rommy Jonns ambae ni Dj wa msanii mkubwa Diamond Platinumz alikutana na kisanga kingine tena cha kubwagiwa mtoto getini kwake ikisemekana kuwa mwanamama huyo alizaa mtoto wa kike na Diamond Platinumz.
Kutoka moja ya mashahidi wanasema kuwa mwanamke huyo aliangaika sana kumtafuta Diamond Platinumz mwenyewe haikufua dafu hivyo aliposikia kuwa mzazi mwenzie na msanii huyo yuko nchini aliamua kuibuka ili kujua hatma yake na mtoto wake.
Majirani wa karibuni na nyumbani kwa msanii huyo walisema kuwa mwanamke huyo na mtoto walikuwa wakilala getii na hata kushambuliwa na mbu usiku kucha lakini walikuwa hawatoki mahali hapo. Hata hivyo baada ya kukutwa usiku na sungusungu waliamua kumchukua na kumpeleka kwa mwenyekiti wa mtaa ili aweze kusaidi wakwa sababu hakuna aliyetaka kumsikiliza.
Baada ya kusikika kwa tetesi hizo kampuni ya habari ya GPL, kupitia gazeti la Risasi waliamua kumtafuta mwenyekiti wa mtaa ambapo anakaa msanii huyo ndipo alipokutana na mjumbe wa nyumba kumi ambae pia alithibitisha kuwepo kwa mwanamama huyo amabe alikuwa akilala pale nje kwa Diamond lakini alisema kuwa hawezi kuongea chochote kwa sababu mwenyekiti yupo kutoa ufafanuzi zaidi.
Mwenyekiti alitafutwa ili kuthibitisha hilo na alisema kuwa “nilitoka nje usiku wa saa nane ambapo tulimhiji na kusema kuwa jina lake ni mama pansheni salama, na alisema kuwa ametoka kenya kuja huku kum=leta mtoto wake kwa baba amabe amezaa nae.
Bahati nzuri kipindi tunaendelea kumhoji diaond mwenyewe alitokea ambapo alitoa kiasi cha shilingi elf 60 ambapo elfu kumi na tano ilitukankwa usafiri wa bajaji mpaka sinza ambapo msanii huyo alituelekeza tumpeleke lakini nyingine alisema ni kwa ajili ya matumizi ya mtoto na mama yake.
Hata hivyo viongozi hao wamekuwa wakilalamika na kusema kuwa wamekuwa wakipta usmbufu sana hata muda mwingine kutumia ela zao za mifukoni ili kuwasaidia na kuwarudisha makwao wanawake wanaokuja kwa ajili ya kuleta watoto wanaosemekana kuwa ni wa msanii huyo, hii sio mara ya kwanza kwa wanawake kuwa wanakwenda kudai haki za matumizi kwa msanii huyo.