Mshindi wa BSS Kuzawadia Milion 50
Kiongozi wa mashindano ya muziki ya BSS Tanzania Madam Ritha ametangaza kuwa zawadi kubwa atakayopewa mshindi ni shilingi milioni 50 za kitanzania ingawa pesa hizo hatopewa zote kwa mara moja.
Madam Ritha anasema kuwa wameamua kutoa pesa hizo kwa awamu kwa sababu kumekuwa na washindi ambao hawanufaiki na pesa hizo hasa wanapokabidhiwa zote kwa mara moja.
Akifafanua kwa undani zaidi, Madam Ritha anasema kuwa Mshindi atakuwa akipewa pesa hizo kila mwezi shilingi mil 1.2 lakini milion 5 za mwanzo atakabidhiwa kwa mara moja siku ya tukio.
Hata hivyo pia msanii huyo aatanza kufanya kazi chini ya Switch Rekodi ambao wameweza kuwakabidhi kwao na tayari walishasaini mkataba tayari.