Msanii mwingine kutoka kenya azuru WCB baada ya Willy Paul
Inaonekana kuwa Willy Paul sio msanii pekee kutoka Kenya ambaye anajulikana na Diamond Platnumz. Siku chache baada ya kuzuru Tanzanian kupromote wimbo wake I Do aliyomshirikisha mrembo kutoka Jamaica, Alaine… msanii mwingine anayejulikana kama Chikuzee kutoka pwani pia alikuwa kwenye ofisi za WCB hivi leo.
Msanii huyu anayejulikana sana pande za Mombasa Chikuzee aka Zee la Mavuvuzela ni alishare picha zake kupitia mitandao yake ya kijamii alipotembelea WCB.
Kwa hivi sasa kuna tetesi kuwa kuna kitu kiko jikoni baina yake na Rayvanny. Mashabiki wake kupitia kwa comments walitaka kujua kama alienda pale kutia sahihi mkataba wa kuwezesha ngoma zake kuwekwa kwenye wasafi.com ama kama walikuwa wanatengeza projects mpya.
Ata hivyo msanii huyu hajafunguka kueleza alikchokuwa akifanya ofisini mwa Diamond Platnumz lakini kuna uwezekano kuwa kuna jambo kubwa wawili hawa wanataka kuachia.