Msamaha wa Babu Seya na Mwanae Waibuka Tena Bungeni.
Desemba 9 mwaka 2017 Mh Raisi Magufuli alitoa msamaha wa rais kwa baaadhi ya wafungwa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali na kati ya wafy=ungwa waliopewa msamaha wa Raisi ni pamoja na Babu Seya na Papii Kocha ambao walikaa jela kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Siku ya jana , moja ya wabunge kutoka chama cha upinzani CUF , aliibuka na kuhoji juu ya msamaha huo na kusema kuwa kwanini wasanii hao walisamehewa ilhali walikuwa wamekutwa na hatia ya kubaka na kulwiti watoto wadogo, hivyo walipaswa kubaki jela kuendelea kutumikia kifungi chao cha kosa walilofanya.
Mtolewa amesema kuwa kitendo alichofanya Raisi cha kukuvali msamaha wa wafungwa hao na kuwapaheshima ya kuwasapoti na kuwapandisha katika majukwaa makubwa nchini ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kusimama tena kimuziki haileti picha nzuri kwa jamii hasa ukizingatia na kosa walilokuwa wamefanya.
kwenye maadhimisho ya uhuru kulitoka kwa msamaha wa wafungwa wakiwemo babu seya na wenzake,ambapo pasipo shaka mahakama ilithibitisha kuwa hawa watu ni wabakaji.sasa tunapotoa msamaha kwa wabakaji tunaweka wapi ulinzi wa watoto wetu.tunawapandisha kwenye majukwaa wafanye show yaani tunawaona nao ni kioo cha jamii je wanafundisha nini?
Mbunge huyo aliongezea kwa kusema kuwa serikali inawaharibu wa toto kwa sababu mwisho wa siku utataka kuwa uliza watoto unandoto za kuwa kama nani katika nchi hii na mtoto hatosita kujibu nataka kuwa mbakaji.
Babu seya na papii kocha walitolewa kwa msamaha wa raisi baada ya kukituumikia kifungo kwa takribani miaka kumi baada ya kukutwa na hatia ya kubaka na kulawiti watoto.Hata hivyo tangu wametoka serikali kupitia wizara ya utamaduni na sanaa wamekuwa mstari wa mbele kuwasaidia na kuhakikisha wasanii hao wanarudi katika mstari wa sanaa.