Msaga Sumu Awashauri Wasanii Wa Singeli Kuwa Na Heshima
Msanii mkali katika muziki aina ya singeli Msaga Sumu amefunguka na kuongea na baadhi ya wasanii wenzie wanaokaa na kudharau wasanii wenzao. Msaga Sumu ambae anafanya vizuri katika aina hiyo mpya ya muziki na imekuja kwa kasi isiyo ya kawaida na kupendwa na watu wengi ameamua kuyaongea hayo kama ushauri kwa wasanii wenzie.
Alipokuwa akiongea katika telesheni ya EATV, Msaga Sumu aliamua kuongea maneno hayo baada ya kusikia baadhi ya maneno kutoka kwa wasanii wenzie ambao kwa muda wamekuwa wakimsema yeye vibaya, msaga sumu anasema kuwa wasanii wenzie wa singeli wamekuwa wakimwambia yeye hajui chochote kuhusu muziki huo wa singeli.
“Wasanii wa singeli mimi naamin wananiponda sana , tena nikikaa kimya hivi ndo wanasema nimefulia kabisaaaa,kumbe mwenzao nipo najitungia sheria zangu huku nikiwaangalia wao , lakini huwa nawaambia ukweli kuwa siki zote kwenye muziki ukiwa na heshima unaweza kufika mbali , kwa kuwa heshima ndio kila kitu” aliongea Msaga Sumu
Hata hivyo Msaga sumu anaonekana kukerwa na baadhi ya wasanii wenzie wa singeli ambao wamekuwa na tabia ya kujiona vichwa na kutokuheshimu wenzao pale tu wanapotoa wimbo mmoja ukafanya vizuri basi wanajiona ndio wameshafika katika muziki na kuanza kuvimba “hawa wasanii wa singeli wengi watafeli muziki kwa sababu heshima hawana, wanajifanya wanavimba vimba na nyimbo moja tu walizokuwa nazo’ ameongezea Msaga Sumu
Msaga Sumu ambae amekuwa akiaaminika kuwa yeye ndio muanzilishi wa muziki huu mpya wa kisingeli ambao unatamba kwa sasa akiutoa katika ngoma za mitaani zinazijulikana kama vigodoro na kufanya wasanii wengine wenye vipaji vya muziki huo kujitokeza.Hata hivyo kwa sasa muziki wa kisingeli umekuwana na wasanii wengi na wanafanya vizuri huku pia mashabiki wakiupokea vizuri sokoni.Haya basi akiwa kama muanzilishi wa muziki huu ameona sio vibaya kuongea na wasanii wenzake ili kufanya aina hii ya muziki usiyumbeyumbe.baadhi ya wasanii wengine wanaofanya vizuri katika muziki huo ni pamoja na Dullah Makabila ,Manfongo na Shollo Mwamba.