Mrembo Nini Akana Mahusiano ya Kimapenzi na Nay wa Mitego
Mwanamuziki wa Bongo fleva mwanadada Nini, amemkana msanii mwenzake Nay wa Mitego mbele ya hadhara na kusema hawana mahusiano yoyote ya kimapenzi zaidi ya urafiki.
Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi nyingi kuwa wasanii hawa wawili wako Kwenye Mahusiano ya kimapenzi fununu hizi zilianza tangu msanii Nini alipomshirikisha Nay kwenye wimbo wake wa ‘Niwe dawa’.
Lakini baada ya tetesi za kipindi kirefu na picha zao kibao kusambaa mtandaoni Nini amemkana Nay na kusema yule ni rafiki tu na Tena mshkaji wa karibu na msanii mwenzake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Kwenye birthday party yake Nini alifunguka yafuatayo kuhusu Mahusiano Yake na Ney:
Ni kitu ambacho always najibu mara nyingi kwamba siko kwenye Mahusiano na Nay yule ni mshkaji wangu ni mtu ambaye tunafanya kazi pamoja tumeamua kufanya kazi lakini maybe ukaribu wetu ndio unafanya watu wahisi sisi wapenzi lakini mshkaji wangu muda mwingi naspend naye lakini ni strictly kikazi zaidi na pia naamini mapenzi yakichanganywa na kazi hakuna Tena kazi”.
Lakini pia Nini amefunguka na kusema ana mpenzi wake ambaye wanapendana lakini hawezi kumtaja kwa sababu sio staa na ni mtu ambaye hapendi kuwekwa wazi hivyo anaheshimu maamuzi yake lakini siku akiwa tayari atamtambulisha na mashabiki zake wote watamjua.