Mrembo Aibuka na Kudai Anatongozwa na Ali Kiba
Video vixen maarufu kunako gemu la Bongo fleva Sasha Kassim ameingia Kwenye headlines baada ya kudaiwa kuleta mtafaruku Kwenye ndoa ya Ali Kiba na Mke wake Amina Khalef.
Global Publishers wanaripoti kuwa Sasha Meseji hizo zilizovuja zilionekana kutoka kwa Kiba kwenda kwa Sasha usiku mnene, jambo ambalo ni hatari kwa jamaa huyo ambaye inasemekana mkewe alijifungua juzikati.
Rafiki wa karibu wa Sasha amefunguka kuhusu meseji za Ali Kiba na Sasha ameiambia
Hivi mnajua kuwa Sasha ana mawasiliano na Kiba na kuna wakati anawasiliana naye mpaka usiku mwingi? “Kama hamuamini, mimi nitawaletea ushahidi wa chatting zao kwani nimezinasa kutoka kwenye simu ya Sasha mwenyewe, hata hivyo Sasha hamtaki Kiba, mkimbana nyinyi kwa njia zenu, atawaeleza ukweli”.
Baada ya Tetesi hizo gazeti la Risasi lilimsaka Sasha na kumhoji kuhusu Tetesi hizo za mawasiliano na Kiba ilhali anajua ameoa Sasha alifunguka:
Sasa akijua kwanimimi najali? Sikia, mimi huyo Kiba simtaki yeye mwenyewe ndio ananisumbua. Tena kwa taarifa yako, sio Kiba tu hata wasanii wengine kibao wa Kibongo wananisumbua kweli siwataki, siwezi kutoka na msanii wa Bongo labda wa mantoni kama Chris Brown hivi”.
Baada ya Tuhuma hizo nzito dhidi ya yake Ali Kiba alisakwa ndipo alipofunguka haya kuhusu tuhuma hizo:
Samahani sina tabia ya kuchati na watu ovyo”.