Mpiga picha wa Diamond Atangaza Kuacha Kazi Rasmi kwa Diamond

Mpiga picha maarufu wa diamond platinumz anaejulikana kama kifesi  ametangaza kuacha kazi rasmi kwa msanii huyo huku sababu yake kuuu akisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa sababu anaona kama bado ana ndoto kubwa zaidi ya aipo sasa na ili awee kufanikiwa basi ni lazima  aache kazi mahala hapo.

kifesi aliamua kuandika walaka mrefu katika ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa kwa mara nyingi sana amekuwa akifanya kazi katika mazingira magumu yasiyoendana na imani yake  na kumlazimu kufanya hivyo hivyo kwa sababu ni kazi , lakini kwa sasa ameamua kuacha kazi ili aweze kumtumiakia Mungu kwanza.

download latest music    

                                              

Lakini bado kumekuwa na mgongano mkubwa juu ya maamuzi hayo ya kifesi na hii  yote ni kutokana na ukweli kwamba siku mbili kabla ya kutangaza kuacha rasmi kwa kazi hiyo, kifesi alimuandikia dimond ushauri juu ya kuachana na zari na kumwambia kuwa zari ndie mwanamke aliyepewa na mungu kitu ambacho wengi wamekuwa wakiona kama swala hilo limemkwaza Diamond na kuamua kumuachisha kazi.

 

Hata hivyo kuhusu mapenzi ya zari na diamond, tangu mwanzo kifesi alionekana kupingana na kila aliyeweza kusapoti kuachana na Zari kwa sababu yeye aliamini kuwa rafiki yake Diamond alipaswa kuwa na Zari kwa sababu ndie mwanamke aliyemfanya kuwa na furaha na mafanikio pia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.