Moni Akumbushia Kutekwa Kwao, Ilikuwa Siku Kama Leo
Msanii wa hip-hop Moni Centrozone amekumbishai siku kama ya leo mwaka uliopita walikuwa katikamatatizo mazito kutokana na kutekwa kwao na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na mmoja wapo akiwa ni Roma mkatoliki.
Kupitia ukurasa wake wa instagram , Moni aliandika kuwa siku kama ya leo imekuwa ikikaa kichwani mwake kila saa na huwa hawezi kuisahau,aliandika”
siku kama ya leo mwaka 2017 watu wasiojulikana walikuja na kuingia studio wakajitambulisha na kutubeba kama kuku,tulifungwa mikono na macho na kisha tukapelekwa umbali mrefu , tukasimama sehemu watu wakiwa wananong’onezana kma dakika 20 kisha tukapelekwa kwenye nyumba ambayo tulikula kisago heavy , mijeledi mateke na marungu kwa mara ya kwanza nilisali sala yangu ya mwisho nikijua ndio mwisho wangu.
Siku tatu baada ya kutekwa kwa wasanii hao tarehe 08 mwezi huo, walipatikana na kupelekwa katika kituo cha polisi cha oysterbay kwa mahojiano zaidi ingawa mpaka leo hakuna lililowekwa wazi kuhusu wasanii hao kutekwa.