Monalisa Athibitisha Kuwa Balozi Wa Duka La Nguo
Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kukiri kuwa yeye ni balozi wa duka kubwa la nguo na hivyo huwa anauza pia.
Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa limemkuta msanii Monalisa akiwa maeneo ya Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya duka Bannat World akiwahudumia wateja kama kawaida.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Monalisa alisema kuwa yupo dukani hapo kwaajili yeye ni balozi wa duka hilo na mara nyingi mwisho wa mwezi wanafanya punguzo la bei hivyo nakuwepo dukani hapo kwaajili ya kuwahudumia wateja wanaokuja hapo.
Niko hapo nawahudumia wateja kama balozi wa Bannat World na mara mwisho wa mwezi nakuwepo hapa nawahudumia wateja” .