Mkude Simba Atoa Jibu Kuhusu Vichekesho Vyake Kuhamia Kwenye Tv
Mchekeshaji anayetamba sana hivi sasa na vituko vyake Mkude Simba amefunguka na kueleza mipango yake ya baadae kuhusu sanaa yake.
Kwa muda mrefu Mkude Simba amekuwa akisikika sana kwenye redio kwani vichekesho vyake vimekuwa vikirushwa Kupitia stesheni ya redio ya EFM.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Mkude SImba aliulizwa kama ana mpango wa kupeleka vichekesho vyake mbele zaidi mpaka Kwenye Tv ambapo alisema hayo ni maamuzi ya mabosi zake:
Hilo ni jambo ambalo lipo ndani, lipo chini ya Boss wangu Majay, Boss wangu Ndaula, Boss wangu, Sebo, siwezi kulizungumza kwa kipindi hiki kwa kuwa Mkude yupo kwenye Radio.
Kwa hiyo kama watumuhitaji aingie kweye TV watasema kwa sababu tulikuwa na radio, tumefungua TV, it means kamba linawezeka ila bado haijawa rasmi”.
Kwa kipindi cha takribani miaka minne sasa Mkudesimba kwa kushirikiana na Stan Bakora na Bwakyila wakuwa wakivunja mbavu za watu kupitia Radio E FM.