Miss Tanzania 2018 Atangaza Kuibuka Kwenye Filamu na Muziki
Miss Tanzania mwaka 2018, Queen Elizabeth Makune ametangaza rasmi kwamba yupo tayari kuingia kwenye filamu za Bongo movie na muziki wa Bongo fleva.
Queen Elizabeth aliibuka kidedea kwenye mashindano ya Miss Tanzania miezi michache iliyopita na kuenda kuiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss world China.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Miss Tanzania amejigamba kuwa atafanya chochote kwa kuwa ana uwezo katika kazi zote alizotaja alisema kuwa, hawezi kujifunga kwenye kitu kimoja na siku zote ana imani kwamba wanaofanikiwa wengi wanafanya vitu zaidi ya kimoja.
Mbali na kuwa Miss Tanzania kwa mwaka huu 2018, niseme tu kwamba mimi ni muigizaji mzuri na ninao uwezo pia wa kuimba. Kwa hiyo siwezi kusema nitafanya muziki au filamu, chochote kitakachokuja mbele yangu nitaanza nacho, hata ujasiriamali pia uko kwenye damu”.
Kuhusu kushindwa kufika mbali kwenye mashindano ya Miss World yaliyofanyika hivi karibuni Sanya nchini China, mrembo huyo hakuwa tayari kuongea lolote akidai haukuwa muda muafaka.